MALI-USALAMA

Mali: Uhasama waibuka tena baada ya mateka kadhaa kuachiliwa Mali

Chini ya wiki moja baada ya kuachiliwa kwa mateka wa Mali na wale kutoka nchi za Magharibi baada ya wapiganaji zaidi ya 200 wa kjihadi, kuachiliwa n amamlaka nchini Mali, yhasama umeanza tena nchini Mali.

Wanajeshi wa Mali katika operesheni kwenye eneo linalounganisha  mipaka mitatu, wakishirikiana na wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane.
Wanajeshi wa Mali katika operesheni kwenye eneo linalounganisha mipaka mitatu, wakishirikiana na wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane. RFI/Coralie Pierret
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mmoja, kundi la wapiganaji la GSIM limedai kuhusika na mashambulizi matatu yaliyotokea Jumane wiki hii katika mkoa wa Mopti.

Kwa upande mwingine, vikosi vya Ufaransa kutoka Operesheni Barkhane vimewakamata watu kadhaa.

Wengi walikuwa na imani kuwa hali hii ya kubadilishana wafungwa na mazungumzo yaliyotangulia vinawezakuchangia kurejesha hali ya utulivu, au kuboresha maridhiano nchini Mali.

Kundi la wapiganaji la GSIM, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu, limedai kuhusika na mashambulizia dhidi ya jeshi la Mali Jumanne wiki hii.

Wanajeshi kumi na moja wa Mali waliuawa: tisa katika shambulio hilo ambalo lililenga kambi ya Sokoura katika eneo la Bankass, kisha wawili katika shambulio la kuvizia dhidi ya wanajeshi waliokuwa wametumwa kusaidia wenzao katika daraja la Parou. Kwa upande wake, jeshi la Mali limesema limewaangamiza magaidi 13 na kuharibu magari mawili wakati wa kujibu mashambulizi hayo.