UN: Corona yasababisha athari kubwa katika uchumi Afrika
Tume ya uchumi katika Umoja wa Mataifa imeelezea masikitiko yake kutokana na kushuka kwa mchango wa kifedha unaotumwa nyumbani na raia wa bara Afrika, hii ikihusishwa pakubwa na athari za janga la Corona kwenye chumi nyingi.
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa tume hiyo, wahamiaji kutoka Afrika wamekuwa waathiriwa wa mdororo wa uchumi unaoendelea kushuhudiwa kwenye mataifa mengi kufuatia janga la Corona.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zimesema kuwa fedha zinazotumwa nyumbani na raia wa Afrika zinatazamiwa kushuka kwa dola bilioni 18 za Marekani, ikilinganishwa na mwaka jana.
Tume hiyo imeonya hali hiyo ni tishio kubwa zaidi kwa mataifa yenye mizozo kwani wanaotegemea msaada huo ni wengi mno. Imeomba taasisi za kifedha kupunguza ada za kutuma fedha hizo na mataifa yaliyoendelea kuwajumuisha wahamiaji kwenye mpango wa msaada kwa jamii, ili kunusuru hali.