MALI-USALAMA

Zaidi ya wanajeshi kumi wauawa katika mashambulio mawili Mali

Mwanajeshi wa jeshi la Mali
Mwanajeshi wa jeshi la Mali 9. REUTERS/Benoit Tessier

Ngome ya kijeshi huko Sokoura, kwenye eneo la Bankass, "liliengwa na shambulio la kigaidi" usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, limesema jeshi, ambalo limeripoti kuwa "wanajeshi tisa waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa ”.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi kilichotumwa eneo la tukio kililengwa na shambulizi lingine la kuvizia, Jumanne asubuhi, na kusababisha vifo vya wanajeshi watatu, kumi kujeruhiwa" na wengine kadhaa hawajulikani waliko, kulingana na taarifa hiyo.

Kwa kipindi cha siku mbili kuanzia Jumatatu usiku hadi Jumanne jeshi la Mali lilikumbwa na mashambulizi mawili. Kwanza liliyolenga kambi yake iliyoko katikati mwa nchi, kilomita kadhaa kutoka mpaka na Burkina Faso. Eneo linalochukuliwa kuwa la kimkakati.

Washambuliaji, wanaoitwa kama "magaidi" kulingana na neneo linalotumiwa na mamlaka, waliwasili kwa miguu na kwa magari. Walishirikiana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

Wanajeshi tisa wa Mali hapo awali waliuawa katika kambi hiyo.