COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Côte d'Ivoire: Upinzani wataka wapiga kura na wanaharakati "kutoshiriki" kampeni za uchaguzi

Zoezi la kutoa kadi za uchaguzi, huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Oktoba 14, 2020.
Zoezi la kutoa kadi za uchaguzi, huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Oktoba 14, 2020. REUTERS/Luc Gnago

Upinzani nchini Côte d'Ivoire umetoa wito kwa wapiga kura na wanaharakati "kususia kikamilifu" kampeni za uchaguzi kwa "njia zote za kisheria".

Matangazo ya kibiashara

Upinzani pia umetoa wito wa "kuzuia shughuli yoyote inayohusiana na uchaguzi" katika taarifa iliyosomwa na mgombea wa chama cha FPI, Pascal Affi N'Guessan, na la Henri Konan Bédié, mgombea mwingine wa chama PDCI aliyeidhinishwa na Mahakama ya Katiba.

Kwa mwezi mmoja mfululizo, upinzani umeendelea kutoa madai yanayoeleweka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wowote. Madai hayo ni pamoja na kuondolewa Alassane Ouattara kwenye orodha ya wagombea. Hatua ya Alassane Ouattara kuwania katika uchaguzi huo kwa muhula wa tatu ni kinyume na Katiba ya nchi, kulingana na upinzani.

Upinzani unalaani "mapinduzi ya uchaguzi" yanayoandaliwa, na unataka kufunguliwa kwa mazungumzo kuhusu madai haya na kambi zote katika siasa nchini Côte d'Ivoire.