COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Kipenga cha kampeni kupulizwa Cote d'Ivoire

Joto la kisiasa laendelea kuitikisa Cote d'Ivoire, wakati huu kampeni za uchaguzi king'oa nanga.
Joto la kisiasa laendelea kuitikisa Cote d'Ivoire, wakati huu kampeni za uchaguzi king'oa nanga. SIA KAMBOU/AFP

Wagombea urais nchini Cote d'Ivoire wanatazamiwa kuanza kampeni za kusaka kura na kunadi sera zao kuanzia leo Alhamisi wakati huu upinzani ukiendeleza maandamano ya kupinga rais Alasanne Outtarra kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Katika kinyang'anyiro hicho, watakaopambana ni wagombea wanne  ambao ni rais Alassane Outtara, rais wa zamani Henri Konan Bedie, aliyekuwa waziri mkuu Pascal Affi N’Guessan na mbunge wa zamani Kouadio Konan Bertin.

Tume ya kikatibu nchini humo iligoma kuwaruhusu wagombea wengine 40 wakiwemo rais wa zamani Laurent Gbagbo na kiongozi wa waasi Guillaume Soro.

Hata hivyo kampeni hizo ziking'oa nanga leo,upinzani umeapa kuendelea na maandamano ya kumtaka rais Outtara kutowania.

Kwa upande wake rais Outtara amekuwa akijitetea kuwa hakuwa na budi kuwania baada ya waziri  mkuu Amadou Gon Coulibaly aliyetazamiwa kumrithi kufariki dunia ghafla.