GUINEA-SIASA-USALAMA

Hali ya wasiwasi yatanda Guinea kabla ya uchaguzi wa urais Oktoba 18

Hali ya wasiwasi inaendela kutanda nchini Guinea, haswa katika kipindi hiki cha hatua za mwisho za kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa urais wenye utata siku ya Jumapili.

Rais wa Jamhuri, Alpha Condé, na kiongozi wa upinzani, Cellou Dalein Diallo, walipokutana kwa mazungumzo huko Conakry, Septemba 1, 2016.
Rais wa Jamhuri, Alpha Condé, na kiongozi wa upinzani, Cellou Dalein Diallo, walipokutana kwa mazungumzo huko Conakry, Septemba 1, 2016. AFP/CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Rais Alpha conde mwenye umri wa miaka 82 na anawania kwa awamu ya tatu , hatua ambayo imepingwa vikali na wanasisasa wa upinzani nchini humo wakiongowa na Cellou Dalein Diallo ambaye amewasili jijini Conakry tayari kwa uchaguzi huo.

Kuna wasiwasi wa kuzimwa kwa mitandao ya kijamii nchini humo.

Hivi karibuni kundi moja la kiraia lilisema makumi ya watu waliuawa nchini Guinea katika maandamano ya machafuko ya kabla ya uchaguzi wa rais utakaofanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Kundi hilo la National Front for the Defence of the Constitution (FNDC) ambalo linakosoa vikali hatua ya Rais wa nchi hiyo Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 ya kuwania urais kwa muhula wa tatu wenye utata wa kisheria lilisema watu 92 waliuawa katika ghasia hizo.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, kundi hilo lilisema miongoni mwa waliouawa, ni raia 45 waliopigwa risasi na maafisa usalama kwa kushiriki maandamano ya kupinga hatua ya Conde ya kuwania urais, yaliyoanzakatikakati ya mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Machafuko hayo yalishtadi mwezi Machi mwaka huu, baada ya kufanyika kura ya maoni iliyomfungulia mlango Conde kugombea muhula huo tata wa urais.

Hata hivyo Waziri wa Usalama wa Guinea, Albert Damantang Camara amepuuzilia mbali madai na takwimu hizo za FNDC akisisitiza kuwa ni za kisiasa na hazina msingi wowote, na kwamba zimetolewa kwa maslahi ya upinzani.