GUINEA-SIASA-USALAMA

Kampeni za uchaguzi zafikia tamati Guinea kabla ya uchaguzi Oktoba 18

Kampeni nchini Guinea imefika tamati kuelekea Uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, huku maafisa wa usalama wakizuiwa watu kuingia katikati ya jiji kuu Conakry bila kutoa sababu yoyote.

Uchaguzi huu unaelezwa kukumbukwa na wasiwasi mkubwa huku ikihofiwa kuwa, huenda mitandao ya kijamii ikazuiwa siku ya Jumapili.
Uchaguzi huu unaelezwa kukumbukwa na wasiwasi mkubwa huku ikihofiwa kuwa, huenda mitandao ya kijamii ikazuiwa siku ya Jumapili. RFI/Carol Valade
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo inashuhudiwa jijini Conakry katika siku ambayo pia kumeripotiwa mauaji ya afisa wa juu wa Polisi katika kambi ya Jeshi, Mashariki mwa jiji la Conaktry.

Maafisa wa polisi wameonekana kwa wingi wakipiga doria katikati ya jiji hilo, huku rais Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 akifanya kampeni ya mwisho kuelekea Uchaguzi huo.

Rais Conde anawania urais kwa muhula wa tatu baada ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuapa kuwania, licha ya kushuhudia maandamano makubwa. Mpinzani wake mkuu ni Cellou Dalein Diallo, Waziri Mkuu wa zamani mwenye umri wa miaka 68.

Uchaguzi huu unaelezwa kukumbukwa na wasiwasi mkubwa huku ikihofiwa kuwa, huenda mitandao ya kijamii ikazuiwa siku ya Jumapili. Raia wa nchi hiyowana hofu kuwa huenda kukatokea machafuko baada ya Uchaguzi huo.