LIBYA-UHAMIAJI-USALAMA

Libya: Afisa wa kikosi cha ulinzi wa baharini akamatwa kwa madai ya kusafirisha wahamiaji

Kikosi cha walinzi wa baharini wa Libya wakipiga doria baharini kati ya miji ya Sabratha na Zawiya, Julai 28, 2017 (picha ya kumbukubu).
Kikosi cha walinzi wa baharini wa Libya wakipiga doria baharini kati ya miji ya Sabratha na Zawiya, Julai 28, 2017 (picha ya kumbukubu). TAHA JAWASHI / AFP

Serikali ya Libya katika jiji laTripoli imetangaza kukamatwa kwa afisa wa kikosi cha ulinzi wa baharini anayeshukiwa kufanya biashara haramu ya wahamiaji kwenda Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Nahodha Abdelrahman Milad - anayejulikana kama "Al-Bidja" - alikuwa afisa mwandamizi wa kikosi cha ulinzi wa baharini huko Zawiya, kilomita 50 magharibi mwa Tripoli. Jina lake liko kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na anatafutwa na polisi ya kimataifa ya Interpol.

Kwa upande wa mwanaharakati wa haki za binadamu wa Eritrea na mwandishi wa habari, Meron Estefanos, ambaye alifanya uchunguzi sana kuhusu biashara haramu ya binadamu nchini Libya, Al-Bidja ni mtu anayejulikana.

"Ukiangalia idadi ya wahamiaji ambao wamepitia Libya - hasa baada ya kuanguka utawala wa Gaddafi - idadi ni kubwa na idadi kubwa ilipita Zawiya ambapo Al-Bidja alikuwa nahodha. Karibu wakimbizi wote ambao nimezungumza nao - na niliwahoji mamia, aiha maelfu - karibu wote wamebaini kwamba afisa huyo alikuwa akihusika na usafirishaji haramu wa wahamiaji, "amesema.

"Lakini ilichukua miaka mingi ili makosa yake yaweze kujulikana. Ajulikana kwa kazi hiyo haramu, ambaye alikuwa akifanya biashara haramu ya vitu vingi, petroli, wahamiaji. Na cha kusikitisha ni kwamba wakati huo huo alikuwa akishiriki katika mazungumzo na nchi za Ulaya juu ya jinsi ya kukomesha uhamiaji haramu. Nimekuwa nikisema kwa miaka kadhaa kuwa kuna maafisa wa kikosi cha ulinzi wa baharini nchini Libya wanaohusika na kusafirisha wahamiaji katika nchi za Ulaya, " ameongeza.

"Ninasubiri kuona wapi atafikishwa mahakamani"

Meron Estefanos anakaribisha hatua ya kukamatwa kwa Al-Bidja. Amesema Al-Bidja anahusika na vifo vya watu wengi.