MALI-USALAMA

Mali: Wakaazi wa Farabougou walasalia nyumbani kwa hofu ya wanajihadi

Picha ya setilaiti ya kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali.
Picha ya setilaiti ya kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali. Google Map

Kwa zaidi ya wiki moja, kijiji cha Farabougou, katika mkoa wa Ségou, kimejitenga na miji mingine nchini Mali, baada ya kuzingirwa na watu wenye silaha ambao hawaruhusu mtu yeyote kuingia au kutoka katika kijiji hicho.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi maarufu katika kijiji hicho wamejaribu kuingilia kati, lakini wakaazi wanaendelea kufungiwa makwao.

“Jeshi tayari limeshafika katika kijiji kidogo, karibu kilometa kumi na kijiji chetu. Watakuja. amesema mkazi huyu wa Farabougou, ambaye anawasiliana na watu wengine kutoka maeneo mbalimbali nchini humo kupitia simu yake ya mkononi. Mkaazi huyu ana imani kuwa suluhu itapatikana, lakini bado anasita kuondoka kijijini humo. Anaogopa uwepo wa "wanajihadi" - na anawaita watu wenye silaha ambao wamefanya uvamizi katika kijiji cha Farabougou zaidi ya wiki moja iliyopita sasa na tangu wakati huo wamewazuia wakaazi wake kuondoka. Wanakijiji wamebaini kwamba watu wasiopungua sita waliuawa na tisa walitekwa nyara wiki iliyopita.

Kulingana na waziri mkuu, jeshi la Mali hata hivyo limeendelea kupiga doria katika siku za hivi karibuni, na linafanya doria kwa kutumia ndege.

Chanzo kimoja cha kijeshi kimesema kuharibika kwa barabara kumechangia pakubwa jeshi kushindwa kufika katika kijiji hicho.