Kiongozi wa upinzani Mauritania Moustapha Ould Limam Chafi arejea nchini
Imechapishwa:
Moustapha Ould Limam Chafi, kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz amerejea nchini tangu Jumapili Oktoba 18, baada ya miaka kumi na moja akiwa uhamishoni nje ya nchi.
Moustapha Ould Limam Chafi alikuwa anatafutwa kufuatia waranti wa kimataifa uliyotolewa na utawala wa rais wa zamani wa Mauritania Ould Abdel Aziz.
Baada ya miaka kumi na moja akiwa ukimbizini nje ya nchi, Moustapha Ould Limam Chafi alirejea nchini jana Jumapili jioni akitumia ndege ya kibinafsi kutoka Doha, mji mkuu wa Qatar, alipokuwa akiishi kwa miaka kadhaa.
Wito wa Limam Chafi, ambaye alikuwa ameomba wafuasi wake kuepuka na mikusanyiko atakaporejea nchini kwa sababu ya janga la Covid-19, hakusikilizwa; Alipokelewa na umati wa wafuasi wake kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nouakchott.
Kati ya wale waliokuwepo, Limam Chafi alikutana na marafiki zake, wakimbizi wa kisiasa wa zamani. Mohamed Ould Bouamatou, mfanyabiashara na bilionea ni mmoja wanasiasa hao wakati wa enzi za Aziz.
Mohamed Ould Bouamatou alirejea nchini mwezi uliopita baada ya muda waranti wa kumatwa dhidi yake kufutwa mwezi Februari. Mwingine, ni kamanda wa zamani wa jeshi Saleh Ould Hanena, ambaye aliongoza uasi wa jeshi dhidi ya rais wa zamani Ould Taya mwaka 2003.