COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Maandamano dhidi ya Ouattara yagharimu maisha ya mtu mmoja

Angalau mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa leo Jumatatu Kusini-Mashariki mwa Cote d'Ivoire wakati wa maandamano mapya dhidi ya rais Alassane Ouattara, ambaye anawania muhula wa tatu katika uchaguzi unaopangwa kufanyika Oktoba 31.

Vurugu hizo zilitokea katika mji wa Bonoua, karibu kilomita hamsini kutoka mji wa Abidjan, wakati vikosi vya usalama vilipowafyatulia risasi waandamanaji, mashahidi kadhaa wamebaini.
Vurugu hizo zilitokea katika mji wa Bonoua, karibu kilomita hamsini kutoka mji wa Abidjan, wakati vikosi vya usalama vilipowafyatulia risasi waandamanaji, mashahidi kadhaa wamebaini. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizo zilitokea katika mji wa Bonoua, karibu kilomita hamsini kutoka mji wa Abidjan, wakati vikosi vya usalama vilipowafyatulia risasi waandamanaji, mashahidi kadhaa wamebaini.

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha waandamanaji wakiwa wamembeba mtu kwenye machela ya chuma.

"Nilimwona kijana aliyeuawa. Wametembea katika eneo hili na mwili wake," amesema Pélagie Vangah, mmoja wa wafanyakazi katika eneo la Bonoua.

Afisa mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kwa upande wake kwamba aliona askari wa polisi wakimpiga risasi mwandamanaji anayepinga serikali. Waandamanaji wengine kadhaa wamejeruhiwa, ameongeza.