MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Wanajihadi waendelea kuweka sheria zao katika kijiji cha Farabougou

Picha ya setilaiti ya kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali.
Picha ya setilaiti ya kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali. Google Map

Ni wiki mbili zimepita tangu wakaazi wa kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali, wameendelea kutengwa na miji mingine. Watu wenye silaha wamepiga marufuku mtu yeyote kuingia katika kijiji hiki kidogo kinachopatikana karibu na mji wa Diabaly, katika mkoa wa Ségou.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuua angalau wakaazi sita na kuwateka nyara wengine tisa wiki mbili zilizopita, kulingana na mashahidi kutoka eneo hilo, wauaji bado wanapiga marufuku watu kutembea katika kijiji hicho.

Haiwezekani kuingia au kutoka katika kijiji hicho. Mwishoni mwa wiki hii iliyopita, daraja linalounganisha kijiji cha Farabougou na miji mingine liliharibiwa.

Kijiji cha Farabougou, katika mkoa wa Ségou, kimejitenga na miji mingine nchini Mali, baada ya kuzingirwa na watu wenye silaha ambao hawaruhusu mtu yeyote kuingia au kutoka katika kijiji hicho, mmoja wa mashahidi amesema.

Chanzo kimoja cha kijeshi kimesema kuharibika kwa barabara kumechangia pakubwa jeshi kushindwa kufika katika kijiji hicho.