DRC-ELIMU

Waalimu waanza mgomo DR Congo

Wanafunzi katika ua wa shule ya ufundi na biashara huko Kinshasa.
Wanafunzi katika ua wa shule ya ufundi na biashara huko Kinshasa. Arsene Mpiana / AFP

Nchini DRC, walimu kutoka chama cha walimu cha SYECO na wale kutoka chama cha walimu wa kikatolika (SYNECAT) wameanza mgomo wao leo Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Wanadai maboresho katika mshahara yao. Wanashuku pia uwepo wa makumi ya maelfu ya walimu hewa kwenye orodha ya malipo.

Baada ya ahadi zilizotolewa hasa na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, hali haibadiliki. Leo Jumatatu, kati ya walimu ambao walmetikia wito wa kugoma na wale ambao wamefanya kazi ya kawaida, madai yao yanafanana.

Walimu wanasema kwamba bado kuna matatizo mengi na mwaka wa masomo haungepaswa kuanza kwa sasa.

Hivi karibuni baadhi ya vyama vya walimu viliamua kusogeza mbele mwaka wa masomo hadi Oktoba 26. Uamuzi ambao ulifutiliwa mbali na mamlaka ya Wizara ya Elimu.

Kwa miaka kadhaa, maelfu ya walimu wamekuwa wanafanya kazi katika shule za umma bila hata kusajiliwa na serikali na wengi wao walikuwa hawalipwi mishahara yao. Ili kutarajia kupata ufadhili wa Benki ya Dunia ya dola milioni 200 mwishoni mwa mwaka huu, serikali inatarajia kuanza kuwalipa. Walimu 58,000 wanatarajia kupokea, kwa mara ya kwanza, mshahara wao mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.