DRC-USALAMA

Wanamgambo wa Kiislamu watorosha wafungwa 900 mashariki mwa DRC

Kati ya wafungwa zaidi ya elfu moja, wafungwa wasiozidi mia moja ndio hawakuweza kutoroka kutokana na shambulio jingine lililotokea kwa wakati mmoja dhidi ya jela la Kangbayi na kambi ya jeshi inayolinda jela hilo, amesema Modeste Bakwanamaha.
Kati ya wafungwa zaidi ya elfu moja, wafungwa wasiozidi mia moja ndio hawakuweza kutoroka kutokana na shambulio jingine lililotokea kwa wakati mmoja dhidi ya jela la Kangbayi na kambi ya jeshi inayolinda jela hilo, amesema Modeste Bakwanamaha. REUTERS

Watu waliojihami kwa bunduki wamefaulu kuwatorosha wafungwa wasiopungua 900 katika shambulio lililoratibiwa asubuhi ya Jumanne dhidi yajela kuu huko Beni, Modeste Bakwanamaha, meya wa mji huo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Modeste Bakwanamaha amelinyooshea kidolea cha lawama kundi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Forces (FDA).

Kati ya wafungwa zaidi ya elfu moja, wafungwa wasiozidi mia moja ndio hawakuweza kutoroka kutokana na shambulio jingine lililotokea kwa wakati mmoja dhidi ya jela la Kangbayi na kambi ya jeshi inayolinda jela hilo, amesema Modeste Bakwanamaha.

"Kwa bahati mbaya, washambuliaji, ambao waliwasili kwa wingi, walifaulu kufungua mlango nguvu kwa kutumia vifaa vya umeme," meya wa mji wa Beni ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu. "Tunaamini kwamba waasi wa FDA ndi walifanya hivyo, " ameongeza.

Kundi la wasi la FDAlinaendesha harakati zake mashariki mwa DRC tangu miaka ya 1990. Limehusika na vifo vya zaidi ya raia elfu moja tangu mapema mwaka 2019, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, licha ya kampeni kadhaa za kujaribu kulitokomeza.

Kundi la Islamic State (IS) limesema shambulio dhidi ya jela huko Beni lilitekelezwa na wapiganaji wa kundi ambalo imelitaja kama mshirika wake katika kanda ya Afrika ya Kati.