DRC-SIASA-USALAMA

DRC: FCC kususia zozei la kuapishwa kwa majaji wa Mahakama ya Katiba

Hatua ya kuapishwa kwa majaji wapya katika Mahakama ya Katiba walioteuliwa hivi karibuni yazua utata katika FCC, muungano vyama vinavyomuunga mkono rais wa zamani Joseph Kabila.
Hatua ya kuapishwa kwa majaji wapya katika Mahakama ya Katiba walioteuliwa hivi karibuni yazua utata katika FCC, muungano vyama vinavyomuunga mkono rais wa zamani Joseph Kabila. TONY KARUMBA / AFP

Mvutano unaendelea nchini DRC kati ya, kwa upande mmoja, spika wa baraza la kitaifa wawakilishi na rais wa bunge la Seneti, na kwa upande mwingine, rais nchi hiyo kuhusu sula la kuapishwa kwa majaji walioteuliwa hivi karibuni katika Mahakama ya Katiba.

Matangazo ya kibiashara

FCC, muungano wa vyama vya kisiasa unaomuunga mkono rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila, FCC umesema kuwa hauwatambui majaji wakuu watatu walioteuliwa na rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi katika Mahakama ya Katiba.

Kauli hii imetolewa wakati rais Tshisekedi atawaapisha rasmi majaji hao hivi leo Jumatano ambapo tayari maspika wa bunge la kitaifa na senate kuunga mkono, huku wabunge wa FCC wametangaza kuwa hawatahudhuria.

Siku ya Jumanne, muungano wa FCC uliwataka wajumbe wake kutoshiriki katika hafla ya kuapishwa kwa majaji wa Mahakama ya Katiba.

Kwa upande wa FCC wanasema, uteuzi wa hivi karibuni kwenye Mahakama ya Katiba unakiuka Katiba. Hoja iliyotolewa na mbunge Théodore Ngoy, ikiungwa mkono na Profesa Nyabirungu Mwene Songa na mawakili wengine kadhaa kutoka kambi ya Kabila.