GUINEA-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais nchini Guinea: Ceni yatangaza matokeo ya awali

Matoto, Matam, Kaloum, katika mkoa wa Conakry na Boffa, katika mkoa wa Boké: katika kila majimbo haya, rais anayemaliza muda wake anaongoza, kulingana na matokeo yaliyochapishwa na Tume ya Uchaguzi.
Matoto, Matam, Kaloum, katika mkoa wa Conakry na Boffa, katika mkoa wa Boké: katika kila majimbo haya, rais anayemaliza muda wake anaongoza, kulingana na matokeo yaliyochapishwa na Tume ya Uchaguzi. JOHN WESSELS / AFP

Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi imeanza tangu jana Jumanne jioni kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Jumapili. Kwa upande wake, chama kikuu cha upinzani cha UFDG, ambacho kinadai kimeshinda kulingana na takwimu zake, kilifanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea utaratibu kitakachotumia.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizo zilitangazwa zinahusu tu Maeneo majimbo, kati ya 38 kwa jumla. Na katika majimbo haya 4, rais anayemaliza muda wake Alpha Condé ndiye anayeongoza.

Matoto, Matam, Kaloum, katika mkoa wa Conakry na Boffa, katika mkoa wa Boké: katika kila majimbo haya, rais anayemaliza muda wake anaongoza, kulingana na matokeo yaliyochapishwa na Tume ya Uchaguzi.

Wakati hou huo, waangalizi wa kimataifa kutoka Umoja wa Afrika na ujumbe wa jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wamesema kuwa uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Guinea Conakry siku ya jumapili iliyopita ulikuwa huru na haki.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Conakry, mkuu wa ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, Waziri Mkuu wa zamani wa Cape Verde José Maria Neves amefahamisha kuwa licha ya kasoro mbalimbali zilizojitokeza, uchaguzi huo ulifanyika katika hali tulivu, huku akiwataka wanasiasa kusubiri matokeo kupitia tume ya Uchaguzi, CENI.

Haya yanajiri wakati hali ya wasiwasi ilishuhudiwa jana katika mji wa Conakry baada ya polisi kuvamia eneo la makazi ya kiongozi wa upinzani Cellou Dallein Diallo aliyejitangaza mshindi wa uchaguzi huo.