DRC-HAKI

DRC: Majaji wapya wa Mahakama ya Katiba wakula kiapo katika FCC na Cach waendelea kugawanyika

Majaji watatu walioteuliwa mwezi Julai waliapishwa Jumatano, Oktoba 21, 2020 mbele ya Rais wa DRC Félix Tshisekedi.
Majaji watatu walioteuliwa mwezi Julai waliapishwa Jumatano, Oktoba 21, 2020 mbele ya Rais wa DRC Félix Tshisekedi. Présidence de la République démocratique du Congo

Majaji wapya watatu wa Mahakama ya Katiba walioteuliwa mwezi Juni wameapishwa Jumatano wiki hii mbele ya rais wa Jamhuri Felix Tshisekedi.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya Bunge. Sherehe hii ilifanyika katika hali ya mvutano kati ya muungano wa CACH, vyama vinavyomuunga mkono rais Felix Tshisekedi, na ule wa FCC, vyama vinavyomuunga mkono aliye kuwa rais wa DRC Joseph Kabila.

Sherehe hizo hazikuhudhuriwa na wanasiasa wa muungano wa FCC unaoungwa mkono na raïs wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila.

Kutohudhuria sherehe hizo kwa maspika wa mabunge yote mawili nchini DRC kumedhihirisha kuwepo kwa mvutano wa kisiasa kati ya muungano wa FCC na ule wa CACH unaoongozwa na rais Felix Tshisekedi.

Wafuasi wa muungano wa CACH walmeombwa kuvunjwa kwa muungano kati ya muungano huo na ule wa FCC serikalini, huku wengine wakiommba mabunge yote mawili yavunjwe haraka iwezekanavyo.

Wengi wamebaini kwamba kuaîshjwa kwa majaji hao ni ushindi mkubwa kwa kambi ya Felix Tshisekedi, huku mshauri mkuu wa rais Tshisekedi katika masuala ya sheria, Nicole Ntumba Bwatshia, akibaini kwamba "yote hayo ni sehemu ya mlolongo wa mageuzi ya katika vyombo vya sheria kama alivyoahidi Mheshimiwa rais wa Jamhuri tangu kuingia kwake madarakani. "