DRC: Félix Tshisekedi kulihutubia taifa, mvutano na waziri wake mkuu waendelea
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi anatarajia kulihutubia taifa leo Ijumaa. Mkutano wa Baraza la Mawaziri ambao ulipangwa kufanyika leo umeahirishwa.
Imechapishwa:
Mvutano bado unaendelea kati muungano wa CACH unaomuunga mkono na ule wa FCC, unaojumuisha vyama vinavyomuunga mkono rais wa zamani Joseph Kabila.
Mvutano huu umeongezeka katika siku mbili zilizopita kufuatia kususiwa kwa sherehe ya kuapishwa kwa majaji watatu wa Mahakama ya Katiba na Waziri Mkuu, Rais wa Bunge la Seneti na spika wa Baraza la Bunge, ambo wote watatu ni kutoka muungano wa FCC, unaojumuisha vyama vinavyomuunga mkono Joseph Kabila.
Nchini DRC, mvutano wa kisiasa bado unaendelea kuhusu kuapishwa kwa majaji 3 walioteuliwa Katika Mahakama ya Katiba na Rais Tshisekedi; Hafla ambayo ilifanyika Jumatano, Oktoba 21.
Muungano huo wa mtangulizi wake unamshutumu rais Felix Tshisekedi kukiuka Katiba kwa kuwateua majaji hao watatu. FCC iliitisha waandishi wa habari jana Alhamisi huko Kinshasa kukemea "udhalimu wa kidikteta" na kuhakikisha kuwa itapinga mpango wowote unaolenga kuzorotesha taasisi na kuendelea na mapambano yake ya kurejesha demokrasia nchini.
Tayari mgawanyiko umejitiokeza katika serikali na wabung, baadhi wanataka wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na rais na wengine wanataka rais ayavunje mabunge yote mawili kwa maslahi ya nchi.