Mali: Jeshi ladhibiti kijiji cha Farabougou kutoka mikononi mwa wanajihadi
Imechapishwa:
Jeshi la Mali limetangaza kwamba limerejesha kwenye himaya yake kijiji cha Farabougou kutoka mikononi mwa wanajihadi. Kijiji hiki chenye wakaazi zaidi ya wakaazi 2,000 kinapatikana katikati mwa nchi hiyo, na kilikuwa kimezingirwa kwa wiki mbili na wapiganaji wa Kiisilamu.
Kijiji cha Farabougou kilianza kuzingirwa baada ya watu kadhaa kutekwa nyara, wengi wao wakiwa wakulima na watu kutoka jamii ya Bambara. Kitendo kilichotekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu.
Shahidi mmoja ameripoti kwamba wanajeshi wa Mali walishindwa kufikia kijiji hicho kutokana na mvua kubwa iliyosababisha barabara kuharibika.
Katika taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa Alhamisi, jeshi lilisema lilipata msaada wa ndege ambazo ziliwawezesha kufika katika eneo hilo lililokuwa limetengwa na miji mingine nchini Mali.