SUDAN-ISRAELI-USHIRIKIANO-AMANI

Israeli na Sudan kufufua uhusiano wao

Donald Trump ametangaza kuanzishwa upya kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israeli na Sudan baada ya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi wa nchi hizo mbili. Oktoba 23, 2020.
Donald Trump ametangaza kuanzishwa upya kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israeli na Sudan baada ya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi wa nchi hizo mbili. Oktoba 23, 2020. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israeli na Sudan, akihakikisha kuwa nchi hizo mbili zimejiunga katika mchakato wa "amani".

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain, Israeli inatarajia kufufua uhusiano wake na nchi ya tatu. Israeli na Sudan tayari zimejiunga katika mchakato wa "amani", ametangaza rais aw Marekani Donald Trump baada ya mazungumzo ya simu na viongozi wa nchi hizo mbili, mazungumzo ambayo waandishi wa habari walihudhuria.

"Rais ametangaza kwamba Sudan na Israeli zilikubaliana kufufua uhusiano wao, hatua mpya kubwa kuelekea amani katika Mashariki ya Kati," amesema msemaji wa serikali ya Marekani.

Donald Trump amehakikisha kuwa mikataba mingine inaandaliwa. "Tuna angalau nchi tano ambazo zinataka kujiunga na (mchakato wa amani) na tutakuwa na nchi nyingi zaidi hivi karibuni zitakazojiunga na mpango huo, " ameongeza Donald Trump.

Tangazo la rais wa Marekani linachukuliwa nchini Israeli kama tukio muhimu katika Mashariki ya Kati, ameripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul. Mabadiliko halisi ya mwelekeo. Miaka hamsini na tatu baada ya Azimio la Khartoum kutangaza mara tatu "hapana" kwa kujiunga na Jumuiya ya nchi za Kiarabu - hapana kwa amani na Israeli, hapana kwa kulitambua taifa la Kiyahudi na hakuna mazungumzo na Israeli - hatimaye Sudan imeeamua kubadili kauli , amesema Benjamin Netanyahu: ndio kwa maneo haya matatu.