VENEZUELA-COLOMBIA

Mpinzani wa Venezuela López akimbilia Colombia

Leopoldo López alifungwa mwaka wa 2014 baada ya kuongoza maandamano dhidi ya rais Nicolas Maduro. Aliachiliwa huru kwa dhamana mwaka 2017.
Leopoldo López alifungwa mwaka wa 2014 baada ya kuongoza maandamano dhidi ya rais Nicolas Maduro. Aliachiliwa huru kwa dhamana mwaka 2017. REUTERS

Mpinzani wa kisiasa nchini Venezuela Leopoldo López ameondoka kwenye makazi ya balozi wa Uhispania huko Caracas na kuitoroka nchi ya Venezuela, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kualikwa huko, vimebaini vyanzo vitatu.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo viwili kati ya ihvyo kimesema Leopoldo López ameelekea Colombia, bila kusema ikiwa tayari amewasili nchini humo.

Leopoldo López alifungwa mwaka wa 2014 baada ya kuongoza maandamano dhidi ya rais Nicolas Maduro. Aliachiliwa huru kwa dhamana mwaka 2017.

Alikuwa mshauri wa kiongozi wa upinzani Juan Guaido, ambaye mwanzoni mwa mwaka jana alitumia katiba ya nchi ili kukaimu nafasi ya rais na kuanza kampeni ya kumpindua Nicolas Maduro.

Baada ya kushindwa kwa jaribio la kijeshi la mwezi Aprili 2019, Leopoldo López alikimbilia katika ubalozi wa Chile, kisha nyumbani kwa balozi wa Uhispania.