GUINEA-SIASA-USALAMA

Guinea: Hali ya wasiwasi bado yatanda Conakry

Askari wakifanya doria katika mji wa Conakry, Oktoba 25, 2020. Jeshi limetakiwa kudumisha utulivu.
Askari wakifanya doria katika mji wa Conakry, Oktoba 25, 2020. Jeshi limetakiwa kudumisha utulivu. Carol Valade/RFI

Hali ya usalama inaendelea bado ni tete katika mji mkuu wa Guinea, Conakry. Makabiliano makali kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yaliripotiwa Jumapili Oktoba 25.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa jumuiya ya kimataifa unajaribu kutuliza hali ya mambo wakati wa siku leo Jumatatu kunafanyika mazungumzo na wadau wote katika mgogoro nchini humo.

Hali ya usalama inatofautiana kutoka mtaa mmoja kwenda mwingine. Vikosi vya ulinzi na usalama vimekuwa vikiendesha ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu Conakry, hususan katika eneo la Kaloum, eneo la kibiashara kunako patikana ofisi nyingi za serikali.

Hivi karibuni Tume ya Uchaguzi nchini Guinea ilimtangaza rais anayemaliza muda wake Alpha Condé kuwa ameibuka mshindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi kwa 59.49% ya kura.

Mpinzani wake Cellou Dalein Diallo, ambaye alijitangaza mshindi wa uchaguzi wa urais kabla ya kutangazwa rasmi kwa matokeo hayo, alipata 33.5% ya kura, kulingana na Tume ya Uchaguzi (CENI).

Tayari mgawanyiko umejitokea katika Tume ya Uchaguzi, CENI.

Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Bano Sow, ambaye ni kutoka upinzani, amesaini tamko linalondekeza " kuanza tena kwa sehemu zoezi au kurejelea upya zoezi la kuhesabu kura kwa sababu ya makosa kadhaa yaliyojitokea katika zoezi la awali.

Ikiwa uchaguzi huu wa urais ulipongezwa na waangalizi wa Kiafrika, ni dhahiri kwamba kasoro nyingi zilijitokeza katika zoezi la kuhesubu kura au wakati wa kukusanya matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo mbalimbali.

Hata hivyo kiongozi wa upinzani Cellou Dalein Diallo amefutilia mbali matokeo hayo na kusema kuwa ni ushindi wa Alpha Conde sio halali, akishtumu Tume ya Uchaguzi, CENI, kumpa kura zisizo halali rais Conde. Ameosema kuwa atawasilisha malalamiko yake mbele ya Mahakama ya Katiba.