GUINEA-SIASA-USALAMA

Maafisa wa Ceni washutumu udanganyifu katika uhesabuji kura Guinea

Mwanamke huyu akiweka kura yake katika sanduku la kupigia kura wakati wa uchaguzi wa urais nchini Guinea huko Conakry Septemba 18, 2020.
Mwanamke huyu akiweka kura yake katika sanduku la kupigia kura wakati wa uchaguzi wa urais nchini Guinea huko Conakry Septemba 18, 2020. AP Photo/Sadak Souici

Siku moja baada ya kutangazwa na Ceni kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi rais anayemaliza muda wake Alpha Conde, mgawanyiko umejitokea katika Tume ya Uchaguzi, CENI.

Matangazo ya kibiashara

Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Bano Sow, ambaye ni kutoka upinzani, amesaini tamko linalondekeza " kuanza tena kwa sehemu zoezi au kurejelea upya zoezi la kuhesabu kura kwa sababu ya makosa kadhaa yaliyojitokea katika zoezi la awali.

Ikiwa uchaguzi huu wa urais ulipongezwa na waangalizi wa Kiafrika, ni dhahiri kwamba kasoro nyingi zilijitokeza katika zoezi la kuhesubu kura au wakati wa kukusanya matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo mbalimbali.

Kukataa kuonyesha matokeo, ukosefu wa uwazi katika kutoa ripoti, kutoweka, kubadilishwa au hata kughushi baadhi ya nyaraka ... Ripoti ya maafisa wa CENI inabainisha "mlolongo wa makosa" yaliojitokeza katika mkoa wa Upper Guinea, unaochukuliwa kuwa ni ngome ya chama tawala ambapo baadhi ya viwango vya ushiriki hubadilika kati ya 98% na zaidi ya 100%. mara kura zilifutwa katika vituo vichache, mara hakuna karibu kura hata moja iliyokuwa batili katika eneo hili la vijijini ambapo kunaripotiwa kiwango cha juu cha watu wasiojua kusoma na kuandika, hati hiyo imebaini.

Wakati wa kujumlisha kura: "Jumla ya kura zilizopigwa zimetofautiana na jumla ya kura wagombea wote walizopata", kulingana na ripoti hiyo ambayo inahoji ukweli wa matokeo na inapendekeza kurejelea upya zoezi la uhesabuji kura.

Mamady 3 Kaba, msemaji wa Ceni, ambaye bado hajapata waraka huo, anasema anaona kuwa umejaa mambo mengi ya uongo wa 'kisiasa'. Wamechelewa, kwa sasa tunasubiri wagombea wanoona kuwa wamefanyiwa dhulma wawasilishe malalamiko yao mbele ya Mahakama ya Katiba, amesema Mamady 3 Kaba.