NIGERIA-MAANDAMANO-USALAMA

Nigeria: Buhari atoa wito wa amani, suala la jeshi kuingilia kati lasalia bila jawabu

Huko Lagos, vijana wakiandamana kwa mamani karibu na jengo la serikali licha ya kutangazwa amri ya kutotoka nje, Oktoba 20, wakipinga vurugu za wanajeshi.
Huko Lagos, vijana wakiandamana kwa mamani karibu na jengo la serikali licha ya kutangazwa amri ya kutotoka nje, Oktoba 20, wakipinga vurugu za wanajeshi. REUTERS/Temilade Adelaja

Serikali ya Nigeria imendelea kuonyesha ishara za kurejesha hali ya utulivu na amani na kutoa taarifa mbalimbali zinazowataka raia kuwa watulivu.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajri baada ya wiki moja ya machafuko kote nchini - ambapo siku ya Jumanne Oktoba 20 vikosi vya jeshi vilitekeleza ukatili dhidi ya waandamanaji walio kuwa wakiandamana kwa amani huko Lagos, na kufuatia na visa vya uporaji na uharibifu katika majimbo mengi.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili jioni, Rais Muhammadu Buhari alitoa "wito wa amani" na kusikitishwa na vifo vya watu wengi nchini Nigeria kufuatia vurugu hizo. Hata hivyo hakutaja au kuishtumu hatua ya jeshi kuzima kikatili maandamano ya watu waliokuwa awkiandamana kwa amani huko Lagos, wiki iliyopita. Hali ambayo ilisababisha vifo vingi na kushtumiwa na nchi nyingi.

Kulingana na maafisa wake wa mawasiliano, Rais Muhammadu Buhari ameamua "kutoingia kwa kina kwenye mjadala" wakati "ukweli wote utakuwa bado haujathibitishwa" kuhusu uingiliaji kati wa jeshi dhidi ya waandamanaji waliokusanyika katika eneo la Lekki.

Kwa upande wake, jeshi la Nigeria linaendelea kukana kabisa kuhusika kwake katika mauaji hayo, hadi kufikia kudai kwamba picha zilizopigwa na waandamanaji walioshiriki maandamano hayo zilikuwa za uwongo.

Siku moja kabla, Gavana Babajide Sanwo-Olu alimpokea mtangulizi wake, Bola Tinubu - na kuzungumza ana kwa ana. Gavana wa zamani wa Jimbo la Lagos na mkuu wa sasa wa APC, chama tawala nchini Nigeria, bila shaka ni mmoja wa watu matajiri na wenye ushawishi mkubwa nchini Nigeria. Bola Tinubu pia anashukiwa kuwa na jukumu katika uingiliaji wa jeshi wiki iliyopita huko Lagos.

"Madai haya ni uwongo kamili na wa kutisha" amejibu Bola Tinubu, ambaye alikuwa amekaa kimya kabisa tangu kuanza kwa maandamano hayo.