SENEGAL-AJALI

Senegal: Wahamiaji zaidi ya 20 wakufa maji baada ya boti lao kuzama

Eneo la uvuvi la Guet N'dar huko Saint-Louis (picha ya kumbukumbu).
Eneo la uvuvi la Guet N'dar huko Saint-Louis (picha ya kumbukumbu). Wikimedia Commons CC by 4.0 / Alweaver2

Watu zaidi ya ishirini wamefariki dunia baada ya boti lao kuzama kutokana na kulipuka kwa inijini. Watu hao ambao wengi wao ni vijana kutoka eneo la Saint-Louis, nchini Senegal, walikuwa wakisafiri kwenda Uhispania kutafuta maisha bora.

Matangazo ya kibiashara

Watu 200 ndio walikuwa wakisafiri kwenye boti hilo, kwa lmujibu wa vyanzo rasmi nchini Senegal.

Taarifa hii imegonga vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini Senegal.

Wakati huo huo rais Macky Sall amebaini kwamba "zaidi ya vijana 20 wamefariki dunia katika ajali hiyo". Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, rais wa Senegal ametoa "salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza ndugu zaoi".

Ajali hiyo ilitokea kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 80 kutoka mji wa Mbour.

Familia na marafiki waendelea kunatafuta taarifa kuhusu wapendwa wao ambao wametoweka.

Jeshi la Senegal linadai kuwa limeokoa "manusura 51". Wengine waliokolewa na wavuvi. Lakini bado ni mapema kujua idadi kamili ya manusura. Jeshi la wanamaji la Senegal linaendelea na operesheni ya kutafuta miili mingine na watu ambao wanawezekana kuwa bado hai katika eneo la tukio, "lakini halijapata maiti hata moja" kwa sasa, limesema jeshi la Senegal katika taarifa.

Huko Saint-Louis, wwakaazi wa eneo hilo wanadai kuwa zaidi ya watu 20 wamekufa maji, kulingana na ushuhuda wa manusura kadhaa.