DRC-MONUSCO-USALAMA

MONUSCO kuhamishia shughuli zake Mashariki mwa DRC

MONUSCO imeamua kuhamishia shughuli zake katika maeneo ambayo makundi yenye silaha yanaendelea kuhatarisha usalama, kama hapa mkoani Kivu ya Kaskazini.
MONUSCO imeamua kuhamishia shughuli zake katika maeneo ambayo makundi yenye silaha yanaendelea kuhatarisha usalama, kama hapa mkoani Kivu ya Kaskazini. ALEXIS HUGUET / AFP

Serikali ya DRC na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, wamewasilisha hati kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayopangilia kuondolewa kwa walinda amani na kuvunja kambi zote za kikosi hicho.

Matangazo ya kibiashara

Mikoa ya kwanza inayohusika ni Kasaï ya Kati ( Kasaï central) na Kasaï. kambi za kikosi cha MONUSCO katika mikoa hiyo zinatarajiwa kufungwa ifikapo mwaka 2021. Halafu, utafuata mkoa wa Tanganyika. Kwa mara nyingine tena, Umoja wa Mataifa unataka kurudi kwenye mikoa mikuu mitatu mashariki mwa nchi.

Kiongozi nambari 2 wa Tume hiyo, anayehusika na masuala ya operesheni, Mmarekani David Gressly, aliielezea hapo jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila baada ya miezi miwili: maafisa 300 wa polisi ya Umoja wa Mataifa ndio watachukuwa nafasi za walinda amani wa mwisho kuondoka Kasaï na Kasaï Central, kwa muda mfupi tu ujao.

“Katika mikoa yote miwili, vikosi vya usalama vya taifa vitasimamia usalama bila sisi. Ninaamini ni rahisi sana. Ninaamini hata kwamba ofisi hizi zitafungwa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka ujao. Hii itatuwezesha, pamoja na mambo mengine, kuelekeza nguvu zetu kwenye mizozo ambayo bado ni muhimu sana katika mikoa ya Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini, " amesema David Gressly.

David Gressly alitembelea kambi ya sasa ya jeshi la DRC, FARDC, huko Semuliki katika wilaya ya Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo walinda amani waliuawa mnamo mwaka 2017. kambi hiyo ilikabidhiwa kwa jeshi la DRC mwezi Februari mwaka huu. Hii ni miongoni mwa mikakati ya Tume ya Umoja wa Mataifa. "Tumepandilia maendeleo ya kambi zingine tano kusaidia FARDC kupata maeneo salama na kushikilia nafasi hizo, " ameongeza David Gressly.