COTE D'IVOIRE-GBAGBO-SIASA-USALAMA

Uchaguzi Côte d'Ivoire: Laurent Gbagbo avunja ukimya na atoa wito wa kuepuka "janga"

Laurent Gbagbo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai huko Hague, Februari 6, 2020.
Laurent Gbagbo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai huko Hague, Februari 6, 2020. Jerry Lampen/Pool via REUTERS

Katika mahojiano na kituo cha TV5Monde, rais wa zamani wa Côte d'Ivoire amethibitisha kwamba yuko upande wa upinzani na anapinga muhula wa tatu wa Alassane Ouattara. Ametoa wito kwa pande zote kujadili ili kuepuka kile aambacho amekiita "janga".

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na TV5Monde, Laurent Gbagbo ameelezea kwanini ameamua kusema hivi sasa, siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais wenye utata.

"Nilipoachiliwa huru, nilisubiri kurejea nchini Côte d'Ivoire ili kuweza kupewa nafasi ya kuzungumza. Lakini leo, tarehe 31 Oktoba inakaribia. Mvutano unaweza kutuingiza katika dimbwi la machafuko. Ikiwa nitakaa kimya, sintokuwa mtu mwenye busara, ” amesema rais huyo wa zamani.

Laurent Gbagbo anasema anaelewa na anaunga mkono hasira ya wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa Alassane Ouattara. "Yeye ndiye alifanya kosa, kwa sababu hakuheshimu Katiba", ameongeza Laurent Gbagbo, ambaye pia amebaini: "Niko upande wa upinzani.

Laurent Gbagbo amesema, "moja ya matatizo ya kisiasa barani Afrika ni kwamba tunaandika nakala bila kujiamini."