TANZANIA- UCHAGUZI 2020

Upinzani wapoteza viti vingi vya ubunge, bunge lijalo kutawaliwa na CCM

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania yaendelea kuchapisha matokeo yakionesha chama tawala kuelekea kupata ushindi mkubwa
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania yaendelea kuchapisha matokeo yakionesha chama tawala kuelekea kupata ushindi mkubwa webscreenshot

Msikilizaji wakati matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania yakiendelea kutolewam tayari kuna kila ishara kuwa vyama vya upinzani kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo vimepoteza idadi kubwa ya wabunge wake katika uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huu ikiwa karibu robo tatu ya kura zote zimeshahesabiwa, matokeo yanaonesha kuwa kuna majimbo mawili pekee ndio yamekwenda kwa upinzani.

 

Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku nchini humo ``Mwananchi`, kati ya majimbo 220 ambayol matokeo yake yametangazwa mpaka sasa, majimbo 118 yameenda kwa chama tawala CCM.

 

Jimbo la Nkasi Kaskazini, limechukuliwa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA, baada ya mgombea wake Aida Khenanm kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Ally Kessy.

 

Chama kingine cha upinzani kilichofanikiwa kupata kiti ni kile cha CUF, ambapo mgombea wake Shemsia Mtamba, aliibuka na ushindi katika jimbo la Mtwara Vijijini, ambapo alimbwaga mgombea wa chama tawala na waziri wa zamani, Hawa Ghasia.

 

Nchi ya Tanzania ina jumla ya majimbo 264 nchi nzima, huku ni majimbo takribani 44 pekee ndiyo yaliyosalia kutangazwa.

 

Wadadisi wa siasa za ukanda wanasema licha ya dosari za uchaguzi zilizoshuhudiwa kwa wazi, upinzani nchini humo una safari ndefu katika kuhamasisha uma kupiga kura na kutambua haki zao za kidemokrasia.

 

Baadhi wakionesha hofu yao kuwa taifa la Tanzania linashuka katika kuwa na demokrasia thabiti.