SENEGAL-AJALI

Wahamiaji wasiopungua 140 waangamia katika pwani ya Senegal

avuvi kwenye pwani ya Senegal, huko Thiaroye, ambapo wahamiaji wamekuwa wakipitia kwa kwenda Uhispania, miaka mingi iliyopita.
avuvi kwenye pwani ya Senegal, huko Thiaroye, ambapo wahamiaji wamekuwa wakipitia kwa kwenda Uhispania, miaka mingi iliyopita. AP Photo/Babacar Dione

Wahamiaji wasiopungua 140 wanaotaka kuingia Ulaya wamezama kwenye pwani ya Senegal wakati boti lao lipowaka moto na kupinduka, na kusababisha ajali mbaya zaidi ya boti iliyorekodiwa mwaka huu, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema.

Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo, iliyokuwa imebeba watu 200, ilizama Jumamosi saa chache baada ya kutoka mji wa Mbour, ulioko karibu kilomita 100 kutoka Dakar, IOM imeongeza.

Video iliyorushwa kwenye vyombo vya habari nchini Senegal inaonyesha boti ya uvuvi, ikiokoa baadhi ya watu, kwenye bahari hiyo.

Katika taarifa yake, IOM imebaini kwamba karibu watu sitini waliokolewa.

Wahamiaji wenye ndoto za kuingia Ulaya ambao wengi wao ni kutoka Afrika Magharibi wameongezeka zaidi ya mara nne tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi karibu 11,000 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha mwaka 2019, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).