CONGO-OPANGO-SIASA-USALAMA

Congo-Brazzaville yatoa heshima za mwisho kwa rais wa zamani Yhombi Opango

Congo imepiga marufu maandamano ya aina yoyote wakati huu nchi hiyo ikiomboleza kifo cha rais wa zamani Yhombi Opango, raia tangu mwaka 1977 hadi 1979, na ambaye aliangushwa mamlakani na rais wa sasa Denis Sassou-Nguesso.

Rais wa Congo-Brazzaville Yhombi Opango huko Paris, mwaka wa 1978.
Rais wa Congo-Brazzaville Yhombi Opango huko Paris, mwaka wa 1978. PIERRE GUILLAUD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu Ijumaa wiki hii bendera za nchi zinapepea nusu mlingoti katika ofisi za serikali na sekta binafsikwa kutoa heshima kwa Jacques Joachim Yhombi Opango, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Alifariki dunia mwishoni mwa mwezi Machi kutokana na Corona nchini Ufaransa, mwili wake ulirejeshwa nyumbani Brazzaville siku ya Alhamisi.

Mwili wa Yhombi Opango umesafirishwa katika kijiji cha Owando, Kaskazini mwa Kongo, ambapo atazikwa Jumamosi hii.