TANZANIA- UCHAGUZI 2020

Magufuli achaguliwa kwa muhula wa pili kwa asilimia 84, upinzani wakataa matokeo

Le président de la Tanzanie, John Magufuli, lors d'un discours à ses partisans le 27 octobre 2020, dans la région de Dodoma.
Le président de la Tanzanie, John Magufuli, lors d'un discours à ses partisans le 27 octobre 2020, dans la région de Dodoma. AP Photo

Rais wa Tanzania, John Magufuli, hapo jana ametangazwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika October 28, ambapo amepata asil imia 84 ya kura zote akifuatiwa na aliyekuwa mpinzani wake Tundu Lissu, kutoka chama kikuu cha upinzani Chadema, aliyepata asilimia 13.

Matangazo ya kibiashara

Hata kabla ya kutangazwa kwa matokeo haya, upinzani ulisema uchaguzi haukuwa wa haki na kwamba hawatambui matokeo yoyote yanayoendelea kutangazwa na tume.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Semistocles Kaijage, idadi ya wapiga kura waliojitokeza ilikuwa asilimia 50.7 katika watu milioni 29 waliokuwa wamejiandikisha.

Kwa upande wa visiwani Zanzibar, tume ya uchaguzi ilimtangaza, Hussein Mwinyi, mgombea wa chama tawala CCM kama mshindi, akimuacha kwa mbali kinara wa upinzanim Seif Sharif Hamad ambaye nae amekataa kutambua matokeo hayo.

Wachambuzi wa masuala ya siasa, wanasema kuanguka kwa upinzani katika uchaguzi huu ni pigo licha ya madai yao ya kuibiwa kura.

Ushindi huu unaendelea kukiweka madarakani chama tawala CCM ambacho kimekuwa kikitawala taiafa hilo tangu Uhuru wake, huku nafasi za ubunge na udiwani zikichukuliwa na chama hicho kwa zaidi ya asilimia 90, upinzani ukipoteza karibu viti vyote ilivyokuwa
navyo.