MALI-USALAMA

Mali: Hali yazidi kuwa mbaya kati ya jeshi la Mali na wanajihadi Farabougou

Picha ya setilaiti ya kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali.
Picha ya setilaiti ya kijiji cha Farabougou, katikati mwa Mali. Google Map

Tangu kuingia kwa jeshi la Mali huko Farabougou, kijiji kinachopatikana katikati mwa Mali ambacho kilikuwa chini ya udhibiti wa wanjihadi, hali ya utulivu ilikuwa ikiripotiwa. Lakini tangu Ijumaa asubuhi, makubaliano haya ya kusitisha uhasama yalivunjika.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wanakijiji 20, au 24 kulingana na maafisa kadhaa seikali katika eneo hilo, walitekwa nyara wakati walikuwa wakivuna katika mashamba mkoani Dogofry, karibu na kijiji cha Farabougou.

Vyanzo vingine pia vinataja kwamba mazao yalichomwa moto, lakini kulingana na afisa moja wa serikali , moto huo chanzo chake bado hakijabainika, ulianzia kwenye nyasi.

Kwa vyovyote vile, huu ndio mwisho wa hali ya utulivu iliyokuwa ikijiri huko Farabougou baada ya kuwasili kwa jeshi la Mali mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hofu ya kuzuka machafuko mengine

Mwanzoni mwa juma, wanajihadi walisema wako tayari kuondoka katika eneo hilo, lakini kwa sharti moja tu: wawindaji wa jadi wajulikano kama Dozo kutoka Farabougou wasalimishe silaha zao. Ba ya jamii hiyo ya wawindaji kukataa kutii ombi hilo, wanajihadi wameanzisha mapambano wakidai kuwa wanataka kuwapokonya silaha wanazozimiliki, mmoja wa wapatanishi amesema.

Kufikia sasa jeshi la Mali halijatoa maelezo zaidi kuhusiana na hali hiyo huko Farabougou.