COTE D'IVOIRE-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Wito wa utulivu kwa uchaguzi wa amani waendelea kutolewa Cote d'Ivoire

Kabla ya uchaguzi wa Oktoba 31, viongozi wa kidini na wasanii wameendelea kutoa wito wa kudumisha utulivu (picha ya kumbukumbu)
Kabla ya uchaguzi wa Oktoba 31, viongozi wa kidini na wasanii wameendelea kutoa wito wa kudumisha utulivu (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Luc Gnago

Wakati raia wa Cote d'Ivoire wakijiandaa kupiga kura kumchagua rais wao Jumamosi hii, Oktoba 31, viongozi wa kidini wameendelea kutoa wito wa kudumisha umoja, huku wasanii wakinadi amani na kuwataka raia kuwa na uvumilivu.

Matangazo ya kibiashara

Wengi wanakumbuka machafuko ya baada ya uchaguzi yaliyoikumba nchi hiyo mwaka 2010. Hata hivyo wana imani kuwa uchaguzi wa sasa utafanyika kwa amani.

Muungano wa kidini kuhusu amani, unaowaleta pamoja wawakilishi wa madhehebu kadhaa, Waislamu na Wakristo nchini Cote d'Ivoire, ulitoa taarifa siku ya Ijumaa alasiri, ukitoa wito wa kudumisha utulivu na kuwataka raia wa nchi hiyo kuendelea kutunza amani.

"Tunadhani kuwa kutoa wito mwingine wa amani siku moja kabla ya uchaguzi ni muhimu," Padri Emile Kelignon Aka, msemaji wa muungano wa kidini kuhusu amani amebaini akihojiwa na mwandishi wetu Jenna Le Bras. Tunaamini njia hii inaweza kuzaa matunda, hasa kutuliza mioyo ya wananchi . "

"Hakuna kilicho juu ya Cote d'Ivoire" ameongeza Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki. Sisi, viongozi wa kidini, tunawasihi wale walio madarakani, upinzani, wananchi wa Cote d'Ivoire tukiwaambia: wekeni kando tamaa za mioyo yenu. Baada ya muda wa mwisho, baada ya uchaguzi, Cote d'Ivoire itaendelea kuwepo na tunahitaji amani ili kuendelea kufanya shughuli zetu, ili tuendelee kuishi. "

Lakini sio wawakilishi wa kidini tu ambao wanataka amani. Wasanii wanne mashuhuri, wanamuziki watatu na mchekeshaji mmoja, wameungana na kutoa wimbo uitwao "Comme un Appel" (Kama ukumbusho) ambapo wanawasihi wananchi wa Cote d'Ivoire kuweka kando tofauti zao.

Mwanamuziki wa miundoko ya Reggae, Kajeem anakumbuka vurugu za mwaka 2010 na ana wasiwasi juu ya mivutano ya wiki za hivi karibuni.

"Migogoro inapoibuka, wengi wanajiuliza ikiwa kwamba watu wamesahau wao ni akina nani, kwamba wamezoea kuishi pamoja na kuchangia baadhi ya vitu na watu wanaowazunguka na kwamba kuna kuwa na aina ya fulani ya wazimu wa muda mfupi ambao unawakumba kwa kutendeana ukatili. Sina uhakika wakile kinachotugawanya lakini kinachotuunganisha zaidi ya yote ni Cote d'Ivoire " , Kajeem amesema.