Uchaguzi Cote d'Ivoire: Outtara aongoza katika uchaguzi wa urais
Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara anaongoza kwa mujibu wa matokeo ya awali ambayo yameanza kutangazwa nchini humo, baada ya wananchi wa taifa hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, kushiriki katika uchgaguzi wa urais.
Imechapishwa:
Ouattara ambaye anaelekea kushinda katika uchaguzi huo uliosusiwa na wapinzani, amepata ushindi wa zaidi ya asimimia 90 Katika WIlaya ambazo kura zimeshahesabiwa.
Tayari chama cha rais huyo mwenye umri wa miaka 78, anayewania urais kwa muhula wa tatu, kimeonya kuwa hakitakuwa tayari kushiriki katika mazungumzo na wapinzani kuunda serikali ya mpito baada ya kususisa uchaguzi huo.
Waangalizi wa ndani wamesema ni asilimlia 23 ya wapiga kura ndio walioshiriki katika zoezi hilo, baada ya wito wa upinzani kutaka wafausi wao kutoshiriki lakini pia baadhi ya barabara kufungwa na wapinzani wa rais Ouattara.
Wakati matokeo yanapoendelea kutangazwa, wagombea wa upinzani Henri Konan Bedie, na Pascal Affi N’Guessan wamedai kuwa watu zaidi ya 30 wameuawa katika machafuko ya kisiasa kuanzia Jumamosi iliyopita.