COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Côte d’Ivoire: Guillaume Soro atoa wito kwa vikosi vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire Guillaume Soro anayeishi nchini Ufaransa, amelitaka jeshi nchini mwake kuchua hatua baada ya rais Allassane Outtara kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu na kuibuka mshindi katika Uchaguzi uliosusiwa na wapinzani wiki iliyopita.

Guillaume Soro, Paris , Septemba 17, 2020.
Guillaume Soro, Paris , Septemba 17, 2020. STEPHANE DE SAKUTIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kupitia mitandao ya kijamii, Soro amesema anaunga mkono harakati za wapinzani ambao wametanagza kuunda serikali ya mpito, huku akisistiza kuwa vyombo vya usalama na taasisi mbalimbali zinastahili kuchukua hatua.

Hata hivyo, naibu msemaji wa serikal,i Mamadou Touré, amesema matamshi ya Waziri huyo Mkuu wa zamani hayakubaliki.

Aidha amesema kuwa Guillaume Soro, hawezi kutumia nchi aliyokimbilia ya Ufaransa kuendelea kuidhalilisha Côte d’Ivoire.

Kwa upande mwingine chama tawala cha RHDP nchini Cote d’Ivoire kimelaani kitendo cha upinzani cha kuundwa kwa serikali ya mpito na kusema kuwa ni kitendo cha uasi kinachoweza kuharibu usalama wa taifa hilo.

Katika mahojiano maalum na RFI idhaa ya Kifaransa, mkurugenzi mkuu wa chama hicho Adama Bictogo amesema mahakama ya katiba pekee ndio itakayoamua.