ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia yatangaza rasmi vita dhidi ya vikosi vya Tigray

Jimbo la Tigray liko kaskazini mwa Ethiopia, kwenye mpaka na Eritrea. Operesheni ya vikosi vya ulinzi na usalama vya Ethiopia ilizinduliwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, usiku wa Jumanne 3 kuamkia Jumatano Novemba 4, ili kupata udhibiti wa jimbo ambalo linataka kujitenga.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Januari 12, 2020 huko Pretoria, Afrika Kusini.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Januari 12, 2020 huko Pretoria, Afrika Kusini. Themba Hadebe/AP Photo
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ya vikosi vya jeshi na usalama vya Ethiopia inatarajia kuendelea. Mawasiliano bado yamekatwa na Jimbo la Tigray. Kwa sasa ni vigumu, kujua hasara iliyotokana na mapigano yanayoendelea.

Vita vya maneno viligeuka haraka kuwa vita vya wazi huko Tigray, kilomita 700 kaskazini mwa mji mkuu Addis Ababa. Pande zote mbili zinabaini kwamba ziko vitani. Kwa upande wa Tigray, mamlaka za mkoa zinahakikishia kuwa kuishi kwa Tigray kunategemea mzozo huu. Kwa upande wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, lengo kuu ni kukiangamiza mara moja na chama tawala cha TPLF huko Tigray. Hakuna mazungumzo kwa sasa, kulingana na jeshi, ingawa vyanzo vya kidiplomasia vinasema pande hizo mbili zimeanza mazungumzo ya siri.

Kwa sasa, ni vigumu kujua hasara kutoka pande zote mbili. Pia ni vigumu kujua hali halisi ya mapigano, kwa sababu mawasiliano yote yamekatwa.

Hata hivyo, kinachojulikana tu ni kwamba mapigano yametokea hasa kwenye mpaka kati ya majimbo ya Tigray na Amhara, kwenye umbali wa kilometa 400, na mapigano makali, hasa karibu na mpaka wa Sudan.