Msumbiji-USALAMA

Ishirini waangamia katika mauaji mapya Kaskazini mwa Msumbiji

Mauaji hayo yalitekelezwa mapema wiki hii katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini. Jumatatu wiki hii, miili ya watu waliouawa ilipatikana katika msitu mmoja huko Kazkazini mwa Msubiji.

Wanajeshi wa Msumbiji Machi 7, 2018 huko Mocimboa da Praia, baada ya shambulio la watu wanaodhaniwa kuwa Waislamu katika mkoa huo.
Wanajeshi wa Msumbiji Machi 7, 2018 huko Mocimboa da Praia, baada ya shambulio la watu wanaodhaniwa kuwa Waislamu katika mkoa huo. ADRIEN BARBIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni katika jimbo hili lenye utajiri mkubwa wa mafuta na linalopakana na Tanzania ambapo waasi wamekuwa watekeleza ghasia kwa miaka mitatu, baada ya kutangaza kujiunga na kundi la Islamic State.

Angalau watu wazima watano na vijana kumi na tano waliuawa kwa kukatwa vichwa na washukiwa wa kundi hilo la wanamgambo wa Kiislamuj.

Shambulio hilo lilitokea wilayani Muidumbe wakati wahanga hao walikuwa wakishiriki katika hafla ya kufundwa. Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mauaji hayo, lakini baadhi ya waangalizi wanasema wanashangazwa na shambulio hili lililohusishwa waasi wa Kiisilamu. Eneo la Cabo Delgado lina Waislamu wengi, lakini katika eneo la Makondé, ambapo mauaji yalitokea, wakaazi wengi ni Wakristo.

Kwa hivyo hiki kilikuwa kitendo cha kuua, kutisha na sio kuajiri kama ilivyotokea mara kwa mara. Mwanzoni mwa mwezi Aprili, wanakijiji (vijana) hamsini na wawili kutoka mkoa huo waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine kuchinjwa. Walikataa kujiunga na kundi hilo la wanamgambo wa Kiislam, na kuchukuliwa hatua ya kuuawa. Vijiji vingine vilishambuliwa, kuporwa na kuteketezwa kwa moto tangu kuanzishwa kwa kundi hili la kijihadi mnamp mwaka 2017. Lengo lao ni kuwatia uoga raia na kujaribu kutenga eneo lao la ukhalifa nchini Msumbiji.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data group, waasi wa Kiisilamu tayari wamehusika na vifo vya watu wasiopungua 2,000 tangu kuwasili kwao nchini Msumbiji na wamesababisha watu 400,000 kuyatoroka makaazi yao nchini humo.