CAMEROON-USALAMA

Kardinali Tumi atekwa nyara kaskazini magharibi mwa Cameroon

Kardinali Christian Tumi mbele ya Kanisa Kuu la Douala mnamo 2004.
Kardinali Christian Tumi mbele ya Kanisa Kuu la Douala mnamo 2004. AFP / I. Sanogo

Taarifa ya utekaji nyara wa Kardinali Christian Tumi imethibitishwa na vyanzo kadhaa vya usalama Kaskazini Magharibi mwa Cameroon. Mfalme wa Kumbo, Fon wa Nso, kiongozi wa maadili ya jadi, pia ametekwa nyara.

Matangazo ya kibiashara

Siku chache zilizopita kundi lenye silaha pia liliwateka nyara walimu wa shule ya msingi huko Kumbo ambao waliachiliwa siku ya Alhamisi, Oktoba 5.

Elie Smith, mshirika wa karibu wa kardinali, aliweza kuzungumza na watekaji nyara kwa njia ya simu.

Kardinali Christian Tumi alitekwa nyara siku ya alhamisi mchana na kundi la watu wenye silaha kwenye barabara iliyo kati ya Bamenda na Kumbo.

Kardinali na Fon, mfalme wa Kumbo, walikamatwa huko Baba, na mmoja wa majenerali wa Amazonia, anayejulikana kwa jina la kivita Chaomao. Nilimwita mtoto wa mfalme wa Kumbo ambaye pia alinithibitishia kuwa ni Chaomao, mchungaji wa zamani, kwa sababu alikuwa akishtumu kwamba Kardinali Tumi aliwahimiza watoto kwenda shule. Kwa sababu kwao, ikiwa shule zitaanza, ni ishara ya kurejea kwa hali ya utulivu, mmoja wa washirika wa karibu wa Kardinali Christian Tumi.