CAMEROON-USALAMA

Cameroon: Kardinali Tumi aachiliwa kutoka mikononi mwa watekaji nyara

Kardinali Christian Tumi aliyedaiwa kutekwa nyara nchini Cameroon, ameachiliwa, kulingana na vyanzo kadhaa. Kardinal Tumialitekwa nyara Alhamisi jioni karibu saa 12 jioni kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, eneo linalozungumza Kiingereza, kwenye barabara inayounganisha mji wa Bamenda na Koumbo.

Kardinali Christian Tumi mbele ya Kanisa Kuu la Douala mnamo 2004.
Kardinali Christian Tumi mbele ya Kanisa Kuu la Douala mnamo 2004. AFP / I. Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa Kardinal Tumi ameachiliwa, watu kumi waliotekwa nyara kwa wakati mmoja na yeye karibu na mji wa Kumbo bado wako mikononi mwa watekaji nyara.

Kufikia kwenye majira ya adhuhuri, Kardinali Tumi alikuwa bado hajawasili katika mji wa Kumbo, lakini vyanzo kadhaa, Askofu Mkuu wa Douala, Samuel Kleda, na pia mshirika wa karibu wa kardinali, wamethibitisha taarifa ya kuachiliwa kwake mapema asubuhi.

Elie Smith, amesema kuwa amefarijika kwa taarifa ya kuachiliwa kwa Kardinali Tumi, kwa sababu alikuwa na wasiwasi juu ya afya yake.

Kardinali Tumi ni maarufu nchini Cameroon kwa jitihada zake za kujaribu kupatanisha wanaharakati wanaotaka kujitenga katika eneo linalozungumza Kiingereza na serikali ya Cameroon.

Askofu Mkuu wa Douala Samuel Kleda ameiambia RFI kwamba aliweza kuzungumza naye wakati wa usiku alipokuwa mikononi mwa watekaji nyara.

Kardinali Tumi aliniambia kwamba hakufanyiwa ukatili, na kwamba alikuwa akiulizwa maswali kadhaa, bila kutoa maelezo zaidi, " amesema Askofu Samuel Kleda.

Dereva wake pia aliachiliwa. Walakini, kwa sasa, watu kumi waliotekwa nyara kwa wakati mmoja na yeye, pamoja na kiongozi wa kimila kutoka Kumbo, bado hawajaachiliwa.