DRC-KATUMBI-SIASA-USALAMA

DRC: Moïse Katumbi arejea Kinshasa

Moïse Katumbi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kinshasa, Ijumaa Novemba 6, 2020.
Moïse Katumbi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kinshasa, Ijumaa Novemba 6, 2020. RFI/Sonia Rolley

Baada ya miaka mitano akiwa mbali na mji mkuu wa DRC, gavana wa zamani wa Katanga Moïse Katumbi aliwasili Ijumaa hii katika uwanja wa ndege wa Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Katanga Moïse Chapwe anatarajiwa leo Jumamosi kukutana kwa mazungumzo na rais Felix Tshisekedi kama sehemu ya mashauriano ya kitaifa yaliyoanza Jumatatu wiki hii.

Hii ni nji ya rais Felix Tshisekedi ya kutafuta kusitisha ushirikiano wa kisiasa na mtangulizi wake Joseph Kabila, katika mukhtadha huu wa mzozo wa kisiasa katika muungano wa CASH-FCC ulioko madarakani.

Wafuasi wa Moïse Katumbi na wanaharakati kutoka vyama vingine walilimiminika kwa wingi kwenye uwanja wa ndege wa Kinshasa jana Ijumaa kumlaki mshirika huyo wa zamani wa Joseph kabila Kabange.

"Nimeitikia wito wa mashauriano yaliyozinduliwa na rais wa jamhuri, kwa sababu nchi iko katika hali ya sntofahamu. Tunapaswa kufanya kazi pamoja, ”alisema Moise Katumbi wakati akishuka kwenye ndege.

Mvutano wa kisiasa unaendelea kati ya muungano serikali wa FCC-CASH.

Msafara wa magari ulipokuwa ukiongozana na Moïse Katumbi alipokuwa akitoka uwanja wa ndege wa Kinshasa.
Msafara wa magari ulipokuwa ukiongozana na Moïse Katumbi alipokuwa akitoka uwanja wa ndege wa Kinshasa. RFI/Sonia Rolley