ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Addis Ababa yaendelea kuikabili Tigray kufuatia uamuzi wake

Mapigano yanaendelea huko Tigray, ambapo jeshi la Ethiopia Jumatano lilizindua mashambulizi ili kurejesha udhibiti wa jimbo hilo, ambalo linataka kujitenga.

Le Premier ministre éthiopien, Abiy Ahmed, lors de sa première conférence de presse, le 25 août 2018, depuis son entrée en fonction, en avril.
Le Premier ministre éthiopien, Abiy Ahmed, lors de sa première conférence de presse, le 25 août 2018, depuis son entrée en fonction, en avril. REUTERS/Kumera Gemechu
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wanajeshi waliamua kujiunga na vikosi vya Tigray, ambao inasemekana walipata silaha kubwa za kivita kutoka wanajeshi hao wa serikali.

Siku ya Ijumaa, hatua mpya ilifikiwa kwa mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na vikosi vya serikali.

Chama tawala katika jimbo la Tigray TPLF kimesema kuwa wako tayari kudungua ndege yoyote au helikopta ya vikosi vya serikali ya Ethiopia itakayo paa juu ya anga ya Tigra.

Hata hivyo vikosi vya serikali vimesema katika taarifa kwamba jimbo la Tigray itakuwa kaburi na sio mahali pa kwenda.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, anafananishwa kwa sasa na Mussolini na kiongozi wa zamani wa Ethiopia, Mengistu, ambao wote kwa pamoja walitekeleza mashambulizi ya mabomu dhidi ya jimbo la Tigray hapo zamani.

Wakati huo huo Wabunge nchini Ethiopia wamepiga kura kubadilisha serikali ya jimbo la Tigray.

Hatua hiyo ya wabunge inamaanisha kuwa, serikali ya jimbo hilo imevunjwa, siku tatu baada ya uongozi wa Addis Ababa, kuanzisha operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la wapiganaji la chama tawala la Tigray People's Liberation Front ambalo limedaiwa kuwa na mpango wa kuzua vita na kwenda kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Adha, hatua hii imekuja wakati huu kukiwa na wasiwasi wa kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kufuatia hatua ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutuma wanajeshi kwenda katika jimbo hilo.

Ahmed amesema hatua hiyo ya jeshi imesaidia pakubwa na kuharibu roketi ambazo zilikuwa na uwezo wa kwenda umbali wa Kilomita 300 kutoka katika jimbo hilo.

Mapigano kati ya uongozi wa Tigray na Addis Ababa ulianza, baada ya jimbo hilo kuamua kupanga na kuwa na Uchaguzi wake wabunge mwezi Septemba na kupuuza hatua ya uongozi wa nchi hiyo kuahirisha zoewi hilo kutokana na janga la Corona.