NIGERIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Hofu yatanda Nigeria kuhusu kutokea kwa mlipuko mpya

Nigeria ilirekodi kesi mpya 300 za Covid-19 Jumatatu, Novemba 9.
Nigeria ilirekodi kesi mpya 300 za Covid-19 Jumatatu, Novemba 9. Reuters/Afolabi Sotunde

Nigeria imeendelea kukabiliwa na ongezeko la visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona. siku ya Jumapili nchi hiyo ilirekodi idadi kubwa ya visa vya maambukizi, sawa na visa 300 vilivyopthibitishwa siku hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni idadi kubwa zaidi ya maambukizi yaliyorekodiwa katika nchi hii yenye watu wengi zaidi barani Afrika tangu mwezi Agosti.

Jiji la Lagos, lenye wakaazi milioni 22, bado ni kitovu cha janga hilo nchini Nigeria.

Katika siku za hivi karibuni, mamlaka imeendelea kuzungumzia kuhusu suala la maambukizi ya virusi vya Corona, lakini, hata hivyo, ikibaini kwamba 'mlipuko mpya kwa Nigeria haiwezekani', na kuongeza kwamba kuna ulazima liepukwe kwa hali yoyote katika mazingira magumu ya kiuchumi.

Miezi miwili baada ya kufunguliwa kwa viwanja vya ndege nchini Nigeria , wafanyakazi walirudi kazini mwishoni mwa mwezi Oktoba na shule nyingi zimefunguliwa.Wakati huo huo mamlaka imeendelea kutoa wito kwa raia kuwa makini na kusambaa kwa ugonjwa huo hatari.