DRC-USALAMA-SIASA

DRC: Makao makuu ya jeshi kuhamia katika kambi ya jeshi ya Kokolo

Kulingana na afisa mwandamizi kutoka makao makuu ya vikosi vya FARDC, makao makuu ya jeshi yanapaswa kuhamishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Kulingana na afisa mwandamizi kutoka makao makuu ya vikosi vya FARDC, makao makuu ya jeshi yanapaswa kuhamishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu. KUDRA MALIRO / AFP

Makao makuu ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yametakiwa kuondoka Mont-Ngaliema, eneo ambalo pia kuna makazi ya rais wa nchi.

Matangazo ya kibiashara

Makao makuu ya FARDC yametakiwa kuhamishiwa kwenye kambi ya jeshi ya Kokolo, Makao Makuu ya jeshi la nchi kavu, kambi kubwa zaidi ya jeshi nchini humo.

Hakuna sababu rasmi zilizotolewa na ofisi ya rais kwa hatua hii ya kushtukiza, wakati bado kunaripotiwa mvutano kati ya Rais Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila.

Uamuzi huu ni kutoka "mamlaka ya juu". Unatakiwa kutekelezwa "bila masharti" kwa sababu "kuna dharura". Hii imeandika kwenye ujumbe kutoka kwa Mkuu wa majeshi ya FARDC, Célestin Mbala, akiutuma hasa kwa wakuu husika wa vitengo mbalimbali vya jeshi.

Hajatoa sababu za agizo hili, ambalo limewashangaza maafisa wengi wa jeshi nchini DRC.

Ikiwa baadhi wanazungumza juu ya "hali ya kutokuaminiana" ya rais kwa maafisa wa ngazi za juu - ambapo wasaidizi wake wanajihusisha na uhusiano wa karibu na rais huyo wa zamani, upane wa wasaidizi wa rais Tshisekedi, wameendelea kubaini kwamba ni kwa "sababu za usalama" na" kimkakati ", bila maelezo zaidi.

Inaaminika kwamba eneo la Mont-Ngaliema kuna vifaa vingi vya jeshi. Kuna Wizara ya Ulinzi, lakini pia makao makuu ya kikosi cha Walinzi wa rais. Na Félix Tshisekedi na familia yake wanashi katika eneo hilo, kwa kukosa makazi rasmi ya rais wa nchi.

Kulingana na afisa mwandamizi kutoka makao makuu ya vikosi vya FARDC, makao makuu ya jeshi yanapaswa kuhamishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.