COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Machafuko yasababisha vifo kadhaa Katikati-Mashariki mwa Côte d'Ivoire

Tangu Jumatatu, Novemba 9, angalau watu kadhaa wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika maeneo kadhaa Katikati Mashariki mwa Côte d'Ivoire.

M'Batto, Daoukro na Elibou miji iliyokumbwa na machafuko mabaya katika muda wa saa 48 zilizopita.
M'Batto, Daoukro na Elibou miji iliyokumbwa na machafuko mabaya katika muda wa saa 48 zilizopita. RFI
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti katika vurugu za kisiasa ambazo zinaendelea kuchochewa kikabila.

Jumanne wiki hii, huko Mbatto, katika eneo la Moronou, wakaazi waliamua kusalia makwao, wakiwa na imani kuwa makabiliano kati ya waandamanaji wanaopinga muhula wa tatu wa rais Alassane Ouattara na vikosi vya usalama. Siku moja kabla, mji huo uliwaka moto. Maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Alassane Ouattara yalibadilika kuwa mapigano kati ya jamii za Agni na Malinke.

Mapigano haya, ambayo hayajawahi kutokea katika jiji hili la lenye wakaazi 30,000, yaligharimu maisha ya angalau watu watatu na 26 kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na walio katika hali mbaya.

Kwa ripoti hii ya awali, vifo vingine viliripotiwa katika mji wa Daoukro, ngome ya Henri Konan Bédié ambayo siku ya Jumanne ilikumbwa na machafuko yaliyoanza tangu Jumatatu wiki hii.

“Kuna vizuizi kila mahali. Hakuna maisha. shughuli zote zimekwama, " amesema shahidi mmoja.

Wanajeshi na polisi wanajaribu kadri wawezavyo kuzuia machafuko yaliyolikumba jiji hilo siku ya Jumatatu. Kulingana na manispaa ya jiji, watu wasiopungua sita waliuawa jana huko Daoukro. Kati yao, mmoja alikatwa kichwa na mwingine alichomwa moto. Watu kadhaa pia wamejeruhiwa, " ameongeza shahidi huyo.

Siku ya Jumatatu, eneo la Elibou, kaskazini magharibi mwa Abidjan, lilikumbwa na machafuko yaliyosababisha vifo vya watu watatu. Maandamano na mivutano pia viliripotiwa huko Yamoussoukro, lakini hakuna vifo vilivyoripotiwa.