CAMEROON-USALAMA

Mfalme wa Kumbo, Kaskazini Magharibi mwa Cameroon aachiliwa

Mfalme wa Kumbo, katika jimbo la Kaskazini-Magharibi mwa Cameroon, kiongozi wa kijadi wa jamii ya Nso, yuko huru tangu Jumanne, Novemba 10 siku kadhaa bada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana.

Kanisa Kuu la Kumbo, kaskazini magharibi mwa Cameroon.
Kanisa Kuu la Kumbo, kaskazini magharibi mwa Cameroon. CC BY-SA 3.0/Wikicommons/Kintong
Matangazo ya kibiashara

Sehm Mbinglo II alikamatwa Alhamisi wiki iliyopita huko Baba, karibu na mji wa Bamenda, na watu waliodai kuwa wanaharakati wanaotaka kujitenga kutoka kundi la "Bui Warriors".

Mfalme wa Kumbo alikutana na mmoja wa wanawe huko Bamenda baada ya siku kadhaa za mazungumzo. Watekaji nyara walikuwa wanadai fidia, ambayo familia yake inadai kwamba haikutoa, na kuondolewa kwa kiongozi huyo wa kijadi kwenye uchaguzi ujao.

Sehm Mbinglo II , mfalme wa Kumbo, alijumuishwa kwenye orodha ya wagombea wa uchaguzi wa chama tawala kwa uchaguzi wa wakuu wa majimbo wa Desemba 6, ucahguzi ambao utakuwa wa kwanza katika historia ya nchi hiyo, ingawa unatajwa katika katiba ya mwaka 1996.

Waasi wa Ambazonia wanapinga kufanyika kwa uchaguzi huo, na ndio sababu walimkamata mfalme wa kumbo, anayestumiwa kwa kuunga mkono ukandamizaji wa serikali katika mikoa inayozungumza lugha ya Kiingereza, wakati alikuwa anarudi Kumbo kwa mara ya kwanza tangu kukimbilia uhamishoni jijini Yaoundé miaka miwili iliyopita, kwa sababu ya ukosefu wa usalama.