MISRI-AJALI-USALAMA

Misri: Saba waangamia katika ajali ya helikopta Sinai

Askari wa Misri katika eneo la Sinai, ambako ajali ya helikopta ilitokea na kuua askari saba wa Kikosi cha Waangalizi wa Kimataifa (MFO).
Askari wa Misri katika eneo la Sinai, ambako ajali ya helikopta ilitokea na kuua askari saba wa Kikosi cha Waangalizi wa Kimataifa (MFO). AFP

Helikopta iliyokuwa ikisafirisha askari wa Kikosi cha Waangalizi wa Kimataifa (MFO) huko Sinai nchini Misri imeanguka Alhamisi, na kuua askari saba, chanzo kutoka Israeli kimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Wamarekani watano, Mfaransa mmoja na askari mmoja wa Jamhuri ya Czech, ni miongoni mwa askari waliopoteza maisha, chanzo hicho kimeongeza.

Ofisi ya MFO nchini Israeli imethibitisha ajali hiyo ya helikopta lakini imekataa kutoa maoni yake kwa kusubiri uchunguzi.

Mpaka sasa hazijafahamika sababu za ajali hiyo, na tayari uchunguzi umeanzishwa kulingana na chanzo hicho kutoka Israel.