ETHIOPIA-USALAMA

Sudan yakabiliwa na wimbi la wakimbizi kutoka Ethiopia

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), lieelezea wasiwasi wake kuhusu mapigano yanayoendelea katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia ambayo yamesababisha raia wengi kutoroka makaazi yao.

Mpiganaji wa kundi la wanamgambo wa Amhara wanaosaidia vikosi vya Ethiopia dhidi ya vikosi vya jimbo la Tigray Novemba 7 huko Musebamb.
Mpiganaji wa kundi la wanamgambo wa Amhara wanaosaidia vikosi vya Ethiopia dhidi ya vikosi vya jimbo la Tigray Novemba 7 huko Musebamb. EDUARDO SOTERAS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika muda wa saa 48, Waethiopia wasiopungua 11,000 walyatoroka makaazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Ethiopia na kukimbilia Mashariki mwa nchi jirani ya Sudan.

Hata hivyo UNHCR imebaini kwamba vita vitaongezeka, na wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Ethiopia linatarajiwa katika siku za hivi karibuni nchini Sudan.

Kikosi cha anga cha Ethiopia kimezindua msururu kadhaa wa uvamizi wa nafasi za Tigrayan wakiwa ardhini, mapigano mazito ya silaha yasemekana yalikutanisha wanajeshi wa shirikisho dhidi ya vikosi vya Tigray Peoples Liberation Front. Mzozo huo umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya wiki moja na

Siku ya Jumatano serikali ya Ethiopia iliwakamata wanajeshi 17 na kuwashtaki kwa kosa la uhani kwa madai ya kushirikiana na uongozi wa jimbo la Tigray.

Hatua hii imekuja baada ya Waziri Mkuu kutuma wanajeshi katika jimbo hilo wiki iliyopita na kuanza kutekeleza mashambulizi kwa kile alichosema uongozi wa jimbo hilo unalenga kuzua machafuko nchini humo.

Shirika la Habari la taifa FBC, liliripoti kuwa, wanajeshi hao waliokamatwa walishirikiana na wapiganaji wa TPLF ili kulishambulia jeshi la taifa.

Aidha, wanajeshi hao wanadaiwa kukata mawasiliano kati ya kambi ya jeshi katika jimbo hilo na makao makuu na mmoja wa wanajeshi hao alikamatwa na vifaa vya mawasiliano pamoja na vilipuzi.

Katika hatua nyingine, Tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia, imelaani kukamatwa kwa wanahabari sita na haijulikani waliko au sababu ya kukamatwa kwao.

Kumekuwa na wasiwasi kuwa huenda operesheni inayoendelea katika jimbo la Tigray ikazua vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko kusambaa zaidi, lakini Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema operesheni hiyo inakaraibia kufika mwisho.