GHANA-SIASA-USALAMA

Kifo cha Jerry Rawlings: Ghana yaomboleza kifo cha rais wake wa zamani

Wakati akivaa barakoa yenye nembo ya chama cha ya chama cha Nana Akufo-Addo (NPP), mfanyabiashara huyu wa mji wa Accra anasema aanasikitishwa na kifo cha Jerry Rawlings, mwanzilishi wa kihistoria wa NDC. "Alikuwa mtu mwaminifu na mwenye busara."
Wakati akivaa barakoa yenye nembo ya chama cha ya chama cha Nana Akufo-Addo (NPP), mfanyabiashara huyu wa mji wa Accra anasema aanasikitishwa na kifo cha Jerry Rawlings, mwanzilishi wa kihistoria wa NDC. "Alikuwa mtu mwaminifu na mwenye busara." RFI/Vincent Pailhé

Jerry Rawlings alikuwa mtu ambaye kupitia kwake Ghana iliingia katika mfumo wa vyama vingi na kuanzishwa kwa demokrasia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa kampeni ya uchaguzi wa urais, Waghana wanaomboleza kifo cha rais wao wa zamani Jerry Rawlings.

Jerry Rawlings, aliyeingia madarakani kufuatia mapinduzi mawili ya kijeshi kabla ya kuanzisha utawala wa kidemokrasia nchini mwake, alifariki dunia Alhamisi asubuhi wiki hii , akiwa na umri wa miaka 73, kulingana na chanzo kutoka ikulu.

Jerry Rawlings, wakati huo akiwa Luteni katika kikosi cha jeshi la wanaanga, alimpindua Jenerali Frederick Akuffo mnamo mwaka 1979 na kuongoza nchi ya Ghana kwa kipindi kifupi na kisha kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia kabla ya kufanya mapinduzi mengine miaka miwili baadaye, akibaini kwamba serikali ilishindwa kukomesha ufisadi na hakukuwa na uongozi bora.

Kuanzia mwaka 1981 hadi 1993, Jerry Rawlings aliongoza serikali iliyoundwa na wanajeshi na raia. Mnamo 1992, alichaguliwa kuwa rais wa Jamhuri chini ya katiba mpya na alichukua madaraka mwaka uliofuata kwa mihula miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa John Kufour mnamo mwaka 2001.

Ripoti kutoka Ghana zinasema kuwa rais huyo wa zamani alifariki hospitalini katika mji mkuu, Accra, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Katika miezi michache ambayo aliongoza nchi mnamo 1979, alikuwa na jukumu la kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya wakuu kadhaa wa zamani wa serikali na majenerali wa jeshi kwa madai ya ufisadi na usimamizi mbaya.

Alionekana pia kama mwokozi wa maskini na alitumia muda wake madarakani kama mtu aliyejitolea.