MALI-UFARANSA-USALAMA

Ufaransa yatangaza kifo cha afisa mwandamizi wa kijihadi nchini Mali

Ufaransa imetangaza kwamba kikosi chake cha barkhane kinachoendelea na harakati zake katika eneo la Sahel na Mali, kimemuangamiza afisa mwandamizi wa kundi la kijihadi Bah Ag Moussa nchini Mali.

Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Barkhane, kinaendelea kukabiliana na makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel, hususan nchini Mali. Makundi ya kijihadi yamesababisha vifo vya watu wengi katika kanda hiyo.
Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Barkhane, kinaendelea kukabiliana na makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel, hususan nchini Mali. Makundi ya kijihadi yamesababisha vifo vya watu wengi katika kanda hiyo. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bah Ag Moussa alikuwa akisakwa sana na jina lake limehusishwa katika miaka ya hivi karibuni na mashambulio mengi katika eneo hilo.

Waziri wa Majeshi wa Ufaransa, Florence Parly, katika taarifa amepongeza operesheni iliyohusisha "taarifa muhimu za ujasusi na vile vile kikosi kilichosaidiwa na helikopta na askari wa nchi kavu" na kutekeleza shambulizi dhidi ya Bah Ag Moussa, ambaye anaelezwa kuwa ni "kiongozi wa jeshi" wa kundi linalotetea Uislamu na Waislamu (GSIM).

Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Barkhane, kimeendelea kukabiliana na makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel, hususan nchini Mali. Makundi ya kijihadi yamesababisha vifo vya watu wengi katika kanda hiyo.