MOROCCO-SAHRAWI-USALAMA

Mvutano katika Sahara Magharibi: Jumuiya ya kimataifa yatoa wito wa utulivu

Kundi la Polisario Front linaalodhibiti eneo lililojitenga la Morocco limetangaza tangu Ijumaa wiki hii kusitishwa kwa mkataba wa usitishwaji mapigano uliofikiwa karibu miaka thelathini iliyopita, mnamo mwaka 1991.

MINURSO (ujumbe wa UN) ulitumwa miaka 25 iliyopita ili kusimamia mkataba wa usitishwaji wa mapigano katika eneo la Sahara Magharibi.
MINURSO (ujumbe wa UN) ulitumwa miaka 25 iliyopita ili kusimamia mkataba wa usitishwaji wa mapigano katika eneo la Sahara Magharibi. Abdelhak Senna / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo lililotolewa baada ya operesheni ya jeshi la Morocco katika eneo la Guerguerat kufungua barabara inayoelekea Mauritania. Umoja wa Mataifa na nchi zinazopakana na Morocco zimejibu zikizitaka pande hasimu kujizuia na mgogoro mwinge unaoweza kuiweka hatarini nchi hiyo.

Mauritania, ambayo wanajeshi wake wameendelea kupelekwa kwa wingi wake na Morocco, imetoa wito kwa wahusika wote kutovunja mkataba wa usitishwaji mapigano.

Kwa upande wa Algeria, inayounga mkono kundi la Polisario Front, imetoa wito wa kukomeshwa kwa operesheni za kijeshi. Waziri wake wa Mambo ya nje, Sabri Boukadoum, amerejelea ombi lake la kuteuliwa kwa mjumbe wa Umoja aw Mataifa, haraka iwezekanavyo, na kuanza tena kwa mazungumzo yaliyositishwa tangu mwezi Machi 2019. Mazungumzo ambayo yanajumuisha Polisario, Morocco, Algeria na Mauritania.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na kuona juhudi zake katika siku za hivi karibuni za kuzuia kuongezeka kwa makabiliano huko Guerguerat zimeshindwa.

Antonio Guterres amesema bado anaazimia kufanya kila liwezekanalo kuzuia kuvunjika kwa mkataba wa usitishwaji mapigano uliofikiwa mnamo mwaka 1991.

Antonio Guterres amepokea barua kutoka kwa uongozi wa Polisario Front ukimtaka apeleke suala hilo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.